Thursday, May 16, 2013

Mashabiki Wa Manchester United Wachanga Fedha Kumrudisha Ronaldo Old Trafford

Cristiano Ronaldo
Baada ya ya mwisho wa wiki ambao ulishuhudia nembo za timu ya Manchester United zikiagwa, nikimaanisha Meneja wa timu hiyo Sir Alex Ferguson na mchezaji mkongwe Paul Scholes, mashabiki wa timu ya Manchester United wanaweza kumkaribisha tena Cristiano Ronaldo - iwapo tu wataweza kusaidia kupatikana kwa hela za kumsajili tena mchezaji huyo.

Bendi moja ndogo ya nchini Australia ambayo ni fuasi wa timu ya United, wameanzisha mtandao maalum ambao mashabiki wa United wanaweza kusaidia kuchangia kwenye mfuko utakaowezesha kupatikana kwa fedha zitakazosaidia kumrudisha aliyekuwa mchezaji wao kipenzi kwenye klabu hiyo.

 
Kwenye mkataba wake wa sasa na timu yake ya Real Madrid, unasema kwamba kwa timu yoyote ambayo inataka kumsajili Cristiano Ronaldo inabidi wagharamike kiasi cha dolla millioni 100 ili iweze kuuvunja.

Kampeni hiyo imepewa jina la 'BringRonaldoHome' imepata wafuasi wengi, huku maelfu ya watu wakitoa ahadi kuweza kufanikisha zoezi hilo, ambapo kwa sasa zimetengenezwa t-sheti za Manchester United zikiwa na picha ya Ronaldo, huku ikielezwa watu zaidi ya milioni kumi wanahitajika kununua t-sheti hizo ili kuweza kufiki lengo hilo.

Mashabiki wa Manchester United wanaweza kuchangia kampeni hiyo kupitia link hii www.bringronaldohome.org/

No comments:

Post a Comment