Wednesday, May 22, 2013

Chris Brown Apata Ajali

Ahhhhh....! Chris Brown, jamaa yani kila kukicha hakosi kutengeneza habari, inakuwa ni kama vile yeye mwenyewe ndiye anayeziandika.

Ila hii hapa kuna habari ya ukweli na wala sio uzushi, juzi kati Breezy alikwaruzana na gari la mtu mwengine, na nataka nikiri kitu kimoja, mara ya kwanza nilipopata habari hii na kwamba ndani ya gari likuwa na Karrueche Tran, akili na mawazo yangu yakaenda moja kwa moja kwa Teddy Pendergrass.

Najua kama nimekuacha kidogo kwenye hili ila unatakiwa uchekeche kichwa japo kidogo.

Hapa nimekuwekea picha za kwenye ajali hiyo, na inaonekana Breezy ndiye ambae hakuwa sahihi. 

Kwani jamaa hana dereva....?
 

No comments:

Post a Comment