Monday, April 29, 2013

Gareth Bale Ashinda Tuzo Mbili Za PFA

Gareth Bale
Winga na mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs na timu ya Taifa ya Wales Gareth Bale, amefanikiwa kushinda tuzo mbili nchini Uingereza, ya kwanza ni ile ya Mchezaji bora wa Mwaka na ya pili ikiwa ni ya mchezaji Chipukizi wa mwaka, tuzo ambazo hutolewa na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa England PFA, huku akiwashinda Luis Suarez wa Liverpool na Robin Van Perse wa Man Uinted.

 Kawaida ya Tuzo hizo mchezaji hupigiwa kura na wachezaji wenzake katika ligi, Bale anakua mchezaji wa Tatu katika historia ya tuzo hizo kuchukua tuzo zote mbili kwa wakati mmoja, huku wa kwanza akiwa Andy Grayambapo msimu wa 1976/1977 akiwa anaichezea Aston Villa na wa pili akiwa ni Cristiano Ronaldo wa Man United msimu wa 2006/2007.

Orodha ya Wachezaji wailoshinda tuzo ya PFA kwa Miaka sita iliyopita hawa hapa:

2012-13: Gareth Bale (Tottenham)
2011-12: Robin van Persie (Arsenal)
2010-11: Gareth Bale (Tottenham)
2009-10: Wayne Rooney (Man Utd)
2008-09: Ryan Giggs (Man Utd)
2007-08: Cristiano Ronaldo (Man Utd)

Kikosi cha Mwaka cha Ligi Kuu ya Uingereza ni hiki:

David de Gea (Manchester United), Pablo Zabaleta (Manchester City), Jan Vertonghen (Tottenham Hotspur), Rio Ferdinand (Manchester United), Leighton Baines (Everton), Michael Carrick (Manchester United), Juan Mata (Chelsea), Gareth Bale (Tottenham Hotspur), Luis Suarez (Liverpool), Eden Hazard (Chelsea), Robin van Persie (Manchester United).

No comments:

Post a Comment