Tuesday, April 16, 2013

AINA MPYA YA CONDOM

Dunia ya sasa imebadilika kwa mengi kutokana na uvumbuzi wa vitu mbalimbali. Kati ya mifano michache kati ya mingi mpaka sasa tumejionea au hata kusikia juu ya magari ambayo yanauwezo wa kujiendesha yenyewe. Swala la Dunia kufanywa kama kijiji kwa kuunganishwa na kompyuta ni kitu mambacho kila mmoja wetu anafahamu. Ndani ya miaka 100, licha ya kuwepo kwa mabadiliko mengi ikiwa ni moja kati ya maendeleo yake, moja kati ya vitu ambavyo havijawahi kuwa nje ya fasheni ni mipira ya kiume (Kondom). Kwa maana toka ilipogundulika na kuanza kutumika mnamo mwaka 1918 muonekano wake umekuwa ni ule ule. Sote tunafahamu kwamba hakunaga muonekano tofauti wa kondum zaidi ya ule ambao kila mmoja wetu anaufahamu miaka nenda rudi, kitu ambacho hakika kinaifanya kuonekana kama sare dunia nzima, huku lengo kuu moja la kujikinga na kuwa na ngono salama. Mtaalamu mmoja aitwae Daniel Resnic anafikiria kuja kufanya mapinduzi juu ya aina mpya ya kondum, na anategemea kuja na ugunduzi mpya utakaoitwa Origami kama inavyoonekana kwenye picha. Kwa mujibu wa mgunduzi huyo, aina hii mpya ya kondomu itakuwa salama na yenye kuleta raha zaidi ya aina ya sasa inayotumika.

No comments:

Post a Comment