Mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na miezi 6 ambaye hajatambulika ni wa nani amekutwa akiwa amefariki dunia kwenye kichakani mara baada ya kutupwa na mtu ambaye hajafahamika mpaka sasa kwenye kijiji cha Mhongolo kilichopo wilayani Kahama.
Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Ally Manyama alieleza kwamba mara baada ya kufika kwenye eneo la tukio alikuta mwili wa mtoto huyo ukiwa umeviringishwa kitenge kisha kutelekezwa kwenye kichakani katika eneo hilo.
Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha.
No comments:
Post a Comment