Tuesday, January 21, 2014

Rais Obama Amesema Bangi ni Nzuri Kuliko Pombe

Rais wa Marekani Barack Obama anaamini kwamba bangi sio kitu hatari ukilinganisha na pombe na kwamba hicho ni kifungo kisichotenda haki kwa baadhi ya watu wengi wenye maisha ya chini waliopo kwenye majimbo mbalimbali nchini Marekani.

Kwenye mahojiano na New Yorker, Rais huyo ameeleza kwamba matumizi ya bangi sio kitu anachoweza kuwashauri watoto wake au mtu yeyoe kutumia, ila tahadhali kimekuwa ni tatizo kubwa ndani ya nchi hiyo.

"Kama ilivyowahi kuelezwa, nilikuwa navuta kama mtoto, na nikaona kuwa ni tabia mbaya na kinyume chake pia, haina tofauti na sigara ambayo niliivuta kama kijana mdogo mpaka nilipofika kuwa mtu mzima. Sidhani kama ni kitu hatari," Bwana Obama alisema.

Bangi imekuwa ni mwiko wa viongozi wengi wa kisiasa, na hata kuna kipindi ilizua matatizo kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Bill Clinton katika kipindi alichokuwa akigombea Urais mnamo mwaka 1992 pale ilipowekwa wazi alikuwa ni mvutaji katika kipindi alichokuwa akisoma nchini Uingereza, na alijibu kuwa hakuwahi na wala kujaribu kufanya hivyo'


Kwa upande mwengine Rais Obama yeye amekuwa mkweli zaidi, akikiri kuwa alikuwa akivuta na hata kutumia cocaine mnamo mwaka 1995 kwenye kumbukumbu za ndoto ya baba yake.

"Nadhani kwamba, kwenye hatua hii, maisha yangu ni kitabu cha wazi, kwa maneno na vitendo.


Wapiga kura wanaweza kufanya maamuzi ya kupotezea mambo ambayo niliwahi kuyafanya katika kipindi nilichokuwa kijana na kulingansha na kazi niliyoifanya toka kipindi kile." -


No comments:

Post a Comment