Saturday, December 14, 2013

Kwa Mara ya Kwanza Ndani ya Miaka 112 Theruji Yaanguka Ndani ya Jiji la Cairo


Watu wengi wanapolifikiri jiji la Cairo hakika watakuwa wanafikiria juu ya mazingira ya joto na vumbi.

Ila kitu kimoja kisichokuwa cha kawaidia kimetokea kwenye eneo hilo usiku - theruji imemwagika.


Kwa mujibu wa waandishi wa ndani wamesema hii ni mara ya kwanza kwa theruji kushuka kwenye mji huo mkuu wa Misri ndani ya miaka 112.

Picha za kushangaza zimeonyesha mji huo ambao mara nyingi huwa ni wenye joto ukiwa umefunikwa na weupe wa theruji.

Wananchi wa Misri walitumia mtandao wa Twitter kuposti baadhi ya picha za hali hiyo ya kushangaza.


No comments:

Post a Comment