Vyanzo
Mazishi ya Nelson Mandela yanaendelea katika kijiji cha Qunu katika mkoa
wa Eastern Cape na kumaliza wiki moja ya maombolezi ya shujaa wa Afrika
mwendazake Nelson Mandela.
Takriban watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa wanahudhuria mazishi hayo ambayo ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa.
Familia ya Mandela ilikesha
wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye atakuwa
anaita mizimu ya mababu wa kale na pia wakiongelesha mwili wa Mandela
kumwambia kuwa sasa anazikwa. Ni kuambatana na tamaduni na mila za watu
wa ukoo wa Mandela wa Thembu.Takriban watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa wanahudhuria mazishi hayo ambayo ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa.
Viongozi wa Afrika, familia na marafiki wametoa heshima zao za mwisho kwa hayati Nelson Mandela katika mazishi yake ya kitaifa katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Cape Mashariki. Mandela alikuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa wakati safari ndefu ya Mandela kuelekea uhuru imekwisha, raia wa Afrika Kusini wana jukumu la kuendeleza sera zake na urithi wake
CHANZO:
MBALIMBALI
No comments:
Post a Comment