Tuesday, July 09, 2013
Tennis: Federer Ashuka Nafasi ya 5, Nadal Sasa Yupo Nafasi ya 4 Kwenye Viwango vya Dunia
Roger Federer ameshuka kwenye horodha ya wacheza tenisi duniani mpaka kwenye nafasi ya tano, hiki ni kiwango cha chini kabisa toka aliposhika nafasi hiyo mnamo tarehe 23 June 2003, wiki mbili kabla hajashinda taji lake la Wimbledon kwa mara ya kwanza kati ya rekodi zake 17 za ushindi wa Grand Slam.
Baada ya kushindwa kuiona wiki ya pili ya michuano ya Wimbledon ya 2013, akitolewa kwenye mashindano ndani ya raundi ya pili na Sergiy Stakhovsky, Federer, 31, sasa ameanguka kwa nafasi mbili chini toka nafasi ya tatu aliyokuwa anashikilia.
Muingereza wa kwanza kutwaa taji hilo toka mwaka 1936, Andy Murray, 26, ameendelea kushika nafasi ya pili, nyuma ya mshindi wa pili wa michuano hiyo kwa mwaka huu Novak Djokovic.
Rafael Nadal, ambaye alishinda taji la French Open, kwa sasa anashika nafasi ya nne nyuma ya Mspanishi mwenzake David Ferrer, ambaye alifika robo fainali.
Serena Williams ambaye alitolewa kwenye michuano hiyo na Mjerumani Sabine Lisicki kwenye raundi ya nne bado anaendelea kuongoza ka upande wa wanawake, akishikilia nafasi ya kwanza ya viwango vya wanawake wacheza tenisi Duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment