Thursday, July 25, 2013

Shuti la Cristiano Ronaldo Lauvunja Mara Mbili Mkono wa Mtoto wa Miaka 11

Charlie Silverwood Mtoto Aliyevunjika
Shuti la mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ilibidi limuache mtoto huyu na maumivu makali mara baada ya mtoto huyu kuvunjika mkono kutokana na mpira kumpiga kwenye mkono wake na kusababisha avunjike.

Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Charlie Silverwood alikuwa amekwenda kushuhudia mechi kati ya timu yake ya Bournemouth ilipokuwa inacheza na Real Madrid kwenye mechi ya kirafiki.

Baba yake alijitahidi kuzuia mpira huo uliopigwa kama free kick na mshambuliaji huyo toka umbali wa mita 35 na kuvuka mpaka kwa mashabiki, shuti ambalo
lilikuwa kama roketi na kwenda kuuvunja mkono wa mtoto huyo mara mbili.

Mtoto huyo alikuwa na shauku ya kuangalia mchezo huo ila ilibidi akose kuishuhudia mechi hiyo kwa dakika 84 zilizobaki baadaa ya kuchukuliwa na kupelekwa hospitali kwa ajili ya kupigwa X-rays ambayo ilitoa majibu ya kuvunjika kwa mkono wake mara mbili.

Ilibidi afanyiwe upasuaji kabla ya kuwekwa bandeji.

Jana Charlie alikiri: “Nilikuwa na maumivu makali, nimewaambia marafiki wakawa hawaamini. Ronaldo ni mchezaji wa gharama zaidi duniani - na amevunja mkono wangu.”


Shuti Lililokwenda Kumgonga Charlie
Baba wa mtoto huyo alisema: “Ni mchezo ambao Charlie hatokuja kuusahau.”

Naye msemaji wa Real Madrid, Juan Camilo Andrade alisema: “Tutachangia gharama za matibabu kwa Charlie.”

No comments:

Post a Comment