Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron |
Waziri mkuu huyo aliyasema hayo alipokutana na mashoga, wasagaji na watetea haki zao ndani ya Downing Street.
Kwanza kabisa Bwana Cameron alielezea ni kwa jinsi gani yeye binafsi anajionea ufahari juu ya mafanikio juu nia yake ya uhalalishwaji huo wa ndoa za namna hiyo duniani kote.
Cameron aliwahi kuwaeleza wageni kwenye sherehe kama hiyo mwaka jana, huku akisema kwamba Uingereza sasa “ni sehemu nzuri kwa mashoga na wasagaji na hata sehemu yoyote ya Ulaya”.
Aliongeza, “kwamba ni mafanikio makubwa. Hiki sio kipimo changu, ni kipimo kinachotambulika kimataifa. Ila bado kuna kazi kubwa ya kufanya.”
Aliongeza pia anataka "kueneza" aina hiyo hiyo ya ndoa Duniani kote ili nchi nyingine zifuate utamaduni huo.
Mwananchi, una lolote la kuchangia..? Basi sema japo neno MOJA tu na Roho yangu itapona...!
No comments:
Post a Comment