Mwanaume ambaye ana malengo ya kuoa hubadilika kitabia. Muda mwingi hutaka kuonekana mtu mzima mwenye sifa nzuri. Hatakuwa mtu wa kulewa kupita kiasi na kutapanya mali na wanawake wengine. Tabia zake mbaya za zamani ataziacha
2. Ataongeza jitihada za
kujitegemea
Mara nyingi wanaume walio
makini na tayari kufunga ndoa, wanahitaji kuwa na kipato cha kutosha kuweza
kuwahudumia wake zao na familia ambazo watakuwa nazo hapo baadaye hivyo
wanajitahidi kutafuta njia za kupandisha hali yao kiuchumi.
Kama ni muajriwa anaweza
akaanza kutafuta miradi mingine nje ya kazi yake ili imsaidie kuongeza kipato
cha kujikimu na hali ya maisha. Kama alikuwa anaishi na wazazi atapanga chumba
na ataanza kujitemea.
3. Anagundua kwamba anahitaji
kuitwa baba
Njia nyingine ya kugundua
mwanaume aliye tayari kwa ndoa ni pale unapotembea naye barabarani,
anawafurahia watoto mnaokutana nao njiani na mara kwa mara ataonekana kukueleza
jinsi atakavyowafanyia watoto wake mara baada ya kuwapata hapo baadaye.
Mwanaume huyo pia huwa na
tabia ya kufurahia maisha ya ndoa ya watu wengine yaani anapomuona mke na mume
wakiwa na mtoto wao basi hutamani sana mngekuwa nyinyi. Mnapotoka hukuita mke
wake!
4. Ni rafiki lakini ni mume
kamili
Mwanaume anayetaka kuoa
anakuwa ni rafiki yako tu kwa sababu hamjafunga ndoa, lakini matendo
anayokufanyia hayana tofauti na yale ya mtu kwa mkewe. Kwa mfano kupanga
mipango ya baadaye ya maisha yenu, kukutambulisha kwa ndugu na rafiki zake. Huwa
na hamu ya kutaka kujua matatizo yako na kukusaidia na wakati mwingine
kukushirikisha katika matatizo yanayomkabili.
5. Hufurahia ukaribu
Mwanaume aliyetayari kuoa
hupenda kuwa karibu na mpenzi wake na asilimia kubwa ya mazungumzo yake
atayaelekeza katika maisha si ngono. Atajitoa kusaidia ndugu wa mke kila
linapokuja tatizo. Na atalalamika anapotengwa na familia ya mchumba wake.
No comments:
Post a Comment