Wednesday, May 15, 2013

Mshambuliaji Wa QPR Loic Remy Ashikiliwa Na Polisi Kwa Kosa La Ubakaji

QPR Loic Remy
Mshambuliaji wa klabu ya Queens Park Rangers ya nchini Uingereza Loic Remy anashikiliwa na Polisi baada ya kutuhumiwa kwa kosa la ubakaji.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anashikiliwa na Polisi wa Scotland sambamba na watu wengine wawili ambao walikamatwa kwenye mji wa Fulham, uliopo Magharibi ya Jiji la London.

Wanatuhumiwa kwa kosa la kumbaka mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 34 mnamo tarehe 6 May.

No comments:

Post a Comment