Bingwa wa mashindano ya mwaka 2015 ya Europa League atapata nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya Ligi ya mabigwa Ulaya, Chama cha Mpira wa Miguu Barani Ulaya kimetaarifu.
Hatua hii imekuja katika hali ya kutaka kuiongezea msisimko michuano hiyo ya pili kwa ukubwa upande wa vilabu.
Maamuzi hayo yamechukuliwa na Mkutano wa Uefa baada ya miezi kadhaa ya majadaliano kati ya Uongozi pamoja na Chama cha Vilabu cha Ulaya.
No comments:
Post a Comment