Sunday, May 19, 2013

Bill Gates Aongoza Kwa Utajiri Duniani

Bill Gates
Muanzilishi wa Redmond, iliyopo Washington-inayojihusisha na kampuni ya Microsoft Corp(MSFT), Bill Gates, amefanikiwa kukamata tena nafasi ya kwanza ya utajiri Duniani kutoka kwa aliyekuwa anashika nafasi hiyo muwekezaji toka Mexico aitwaye Carlos Slim hapo jana.

Kwa mujibu wa horodha ya Mabilionea wa Bloomberg, mtengenezaji huyo wa software toka nchini Marekani Bill Gates, amekamata tena nafasi hiyo baada ya biashara zake za software kupanda chati ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Hii ni mara ya kwanza kwa Gates kushika nafasi hiyo toka mara ya mwisho alipoikamata mnamo mwaka 2007.

Slim anayemiliki America Movil (AMXL) SAB, kampuni kubwa ya simu ndani ya Marekani, ameshuka kwa asilimia 14 mwaka huu baada ya Bunge la Mexico kupitisha muswada ambao unazuia soko billionea huyo. Kitu kilichopelekea kufuta zaidi ya dolla billioni 3 kutoka kwenye utajiri wa jamaa huyo mwenye umri wa miaka 73 sasa.

No comments:

Post a Comment