Afande Sele Na Mama Tunda |
Ni msanii wa Bongo Fleva muite Afande Sele, kwenye picha akiwa na Mama Tunda (Mke Wake)
Hewani kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya uitwao "Dini Tumeletewa" aliomshirikisha mkali wa RnB za kibongo Belle 9.Picha hii nimeikuta kwenye moja kati ya album za Mfalme Sele kwenye Facebook.
Kwenye picha hiyo chini
yake Afande ameandika maneno haya:
"Mfalme Selemani II & Mama Tundajema/Sanaa.
LIVES & LOVES, LIVITY IN
NATURAL PHILOSOPHY, NATURAL ONE..
karibuni."
Mmoja kati ya wasanii wachache ambao hutumia sanaa yake kufikisha ujumbe mzito kwa jamii, sielewe sababu hasa ni nini ila naamini ni uwazi na ukweli wa vitu ambavyo huvizungumza, hakika ni ukweli wa moyoni kwa baadhi ya watu, kitu ambacho watanzania wengi hutopenda aina hiyo ya uandishi sababu inawagusa kwa namna ya kipekee.
Kama huamini hebu fanya kusikiliza wimbo wake mpya unaoitwa "Dini Tumeletewa", wimbo ambao amemshirikisha msanii mwenzake toka Morogoro Belle 9, nina hakika utapata kitu cha kujifunza toka kwenye wimbo huo.
Japo neno moja tu, kwa picha hii na kile utakachokuwa umekipata toka kwenye wimbo huo, tupiamo kwa Afande Sele.....
No comments:
Post a Comment